KWANINI TUNAJIDANGANYA TUNAFIKIRI TUNAPASWA KUWA TOFAUTI KULIKO TULIVYO SASA

Muda mwingi picha yetu ya tutavyokuwa inakuwa mbele ya matamanio yetu kuliko jinsi tulivyo sasa. Mimi wa sasa hana maana sawa na mimi nitayekuja kuwa anavutia zaidi na kuwa na shauku kumfikia. 

Kwanini huwa tunajihisi upungufu kwenye wakati uliopo na kuona nina hitaji kujijaza ili nifikie kuanza kuishi. Je, nikweli tuna upungufu au tumetengenezewa huu upungufu?

Upungufu wetu wakujikataa katika wakati uliopo umeletwa na nini?. Ni kweli Jamii imeshatuandalia sura ya tunavyopaswa kuwa ili tuwe kamili na tutafsirike furaha na amani ndani yetu kwa  kuishi bila maumivu wala shida yoyote ndani yetu ya mateso inayo tuepusha nayo. 

Je, ni kweli kuna maisha yaliyokamilika mbele yetu au sisi aliye tofauti na sasa mwenye ukamilifu. Muda wote wakati uliopo umekuwa ukitumika kama daraja tu na kuwa hauna maana sana kama wakati ujao tulivyo na hamu nao. 

Ni kipi kikubwa tunacho kikimbia katika wakati uliopo ambacho hakitakuwepo kwenye sisi wa wakati ujao?. Ina onekana kama jinsi tulivyo umbwa tupo kwenye upungufu ambao jamii yetu imetengeneza njia ya kutufanya tuushinde na kufikia kuishi kwenye lengo iliyo tuandalia ya sisi aliye kamili na kutambulika. 

Hichi kitu kinatufanya tushindwe kabisa na tuwe mbali na jinsi kujitambua tulivyo umbwa?. Hatuna muda wa sisi wenyewe kujiona tuna mbegu gani tuliyobeba ndani yetu bali muda wote tunatazama njee kutafuta nimeambiwa kipi kitakacho nifikisha kwenye kuishi salama kwa jinsi nilivyo fundishwa na jamii. Mbegu yenye kuzalisha matendo yako yakukunufaisha  wewe na ulimwengu wako kama kipawa chako ipo ndani yako na si kuitafuta nnje yako. 

Kitu kikubwa kinachotufanya tunashindwa kujitambua ni tunahofu na kukutana na ukweli wa jinsi tulivyo na kukubaliana nao kiuhalisia. Tunahisi hatupaswi kuwa kwenye upande wa kushindwa, kuumia, kuonekana kinyume na lengo linalokimbizwa na wengi, tunashindwa kusimama na utambulishi wetu halisi unakuwa ni mzigo mkubwa kuwa original na tunakuwa kivuli cha jamii inavyotaka tuwe. 

Mlango wa kwanza wa kufungua katika kujitambua ni kuelewa huwezi ukajifunza kitu chochote kwenye kitu ambacho unataka kukiepuka au kuwa tofauti nacho kukibadilisha. Lazima ujiangalie kama kitu cha dhamani kwa umakini wote kwa vyovyote vile utavyojihisi na kupata mawazo na miitikio ya jinsi ulivyo bila kutaka kuepuka wala kubadilisha chochote kuwa zaidi. Kuwe hakuna usawa unaoutafuta wala ubaya unao ufuta ni wewe unae elea kwenye ufahamu wako na kila kitu kitabadilika kuanzia hapo. 

Huwezi kupata mabadiliko ya ndani kwakufikiria kimawazo tu lazima mabadiliko yaletwe na utambuzi wakuona ukweli wa uhalisia wako. 

Kwa ujumla hali ya maisha ya binadamu haitatuliki kwakuwa sio tatizo, jinsi kufikiri kuwa ni tatizo ambalo unaweza kulimaliza na ukaishi bila changamoto, kuumia au kujihisi usivyopenda, hakuna lengo lolote utalofikia likatatua hilo.  Kuelewa na kuishi kamili kwenye wakati uliopo bila kuuhisi ni tatizo ni njia nzuri ya kufungua uelewa wako kuumiliki wakati wako. 

Lengo kubwa ni kuweza kukufanya uweze kufikiri jinsi gani ninaweza kuonyeshe kilichopo ndani yangu chote na kwa ukweli nyakati zote na kupokea hisia zote za matokea kama yalivyo. Na si kukimbilia kufanya kitu kisicho na ukweli ndani yako kwa lengo tu kina ahadi ya kukupa usalama wa nnje na kuonekana mshindi uliyeshinda upande wa maumivu. 

Jiulize kwanini tunamahusiano mabaya na hisia zetu tunazo ziita za maumivu na kushindwa. Je, Itakuwaje kama utaishi kwa ufahamu na hisia zako kwa kuzitambua maana yake na matendo yako yasiwe  kuzikimbia na kuziepuka kufikiria ni jambo baya kwako la kuliepuka. 

Nb: Kuwa na hisia tofauti na upendavyo haimanishi una upungufu unaotakiwa utokomeze ndani yako, bali ni jinsi mwili unaonyesha utofauti wa tafsiri za matukio ndani yako. Tunapaswa tuache hii tabia ya kutokuwa kamili kwenye wakati uliopo na kufikiria wakati ujao kuna vitu vingi vinatupita na ndio maisha yenyewe yalipo. 


Comments