JE, MAISHA YA KIROHO YANAHUSISHA DINI YOYOTE


Tumezoea kuishi kwenye kufuata muongozo au kanuni ili tujiweke kwenye kipimo cha usalama wa kuwa kwenye usawa. Na ni hivyo huwa maisha ya kiroho tumeyaweka kwenye mabano fulani ukiwa ndani yake unaweza kuhesabika kuyaishi. 

Kwanini kila mtu anayatafuta maisha ya kiroho tuliyo tafsiriwa, kuna sababu kubwa inayo tuvutia na kutupa kimbilio la kufikia hilo kama ni usalama kwetu. 

Je, Maisha ya kiroho yanatokana na mfumo wa dini yoyote au yanatokana na mfumo wowote na si nnje ya hapo?. Dini nyingi zime unganisha kufuata kanuni fulani kwa usahihi ili kuonyesha upo kwenye matakwa sahihi bila kwenda nnje ya hapo na hapo utakuwa kiroho.

Ina maana gani tukisema roho je, ni tofauti na ukawaida wetu. Kwanini kuwe na utofauti wa kuishi kati ya kiroho na kawaida.  Je, kuna kitu tuna kikosa chenye nguvu ya kutuweka kamili kwenye kuishi kawaida. 

Wakati tumezaliwa ni tayari roho yetu kama uzima tuliousimamia ni utambulisho wetu lakini akili inapokuja na mazingira inatutengenezea utambulisho tofauti na kujisahau kabisa asili yetu ya kiroho na hapo ndio mwanzo wa kupoteza nguvu yetu kubwa na kuhangaikia utambulisho wa akili kwa ujumla wa mwili kwakuchukua utambulisho wetu na kutokuwa na uzima na maelewano ndani yetu huwa kuna anzia hapo. 

Kutoelewa kwetu utambulisho wa akili na mwili huwa unatutesa sana na tunafikia hata kuuchoka na kuhitaji hata usinge kuwepo. Dini nyingi zimeweka kujikataa miitikio yako ya kimwili na akili na kuhisi kama inatoka kwa shetani na inahitaji kuiepuka ili upate uhuru kwenye roho yako, na wengine hufikiri kuishi kiroho ni umeweza kuifuta kabisa miititikio ya mwili na akili yako kwa msaada  kutoka juu na kunasiku hilo litatimia ili uwe huru, hii si kweli kabisa ni njia isiyo kufikisha kuweka huru uzima wa roho yako.

 Hata wote wanao kupa mfumo kuhusu hilo hawawezi kuukimbia mwitikio wa mwili wao wala akili yao kwa kuukataa kwa njia yoyote ni jinsi tulivyo ila kuna kitu tunacho kikosa cha muhimu kuweza kuweka huru uzima wa kuishi kiroho kweli ndani yetu. 

Roho ndio mwangaza na maana ya maisha ndani yetu, endapo tutataka kuishi kiroho cha kwanza ni kurudi ndani yetu na si kutafuta mfumo wa kuidhiibiti mifumo yetu mingine ili isiende kinyume tunavyohisi si sahihi kuwa. Hili halipingiki hakuna mtu yeyote nnje yako atayeweza kufikisha uelewa na amani ya kweli ndani yako zaidi ya wewe mwenyewe kuweza kufanya hilo kwa kukubali kujitambua kama ulivyo bila kujihesabu kama tatizo kwako mwenyewe. 

Roho ni ufahamu na uelewa unao kuunganisha na ulimwengu wote, kuweza kuishi kiroho ni kuwa huru ndani yako kwa kuwa na ufahamu kamili wa jinsi akili yako, mwili wako na vyote jinsi ulivyo, kuwa kwenye mwangaza wa roho au ufahamu wa juu na kutokuwa mgeni ndani yako kwa jinsi ulivyo. Hili huambatana na kuacha kujitafsiri kama miitikio ya akili na mwili unayohisi ni tatizo la kulitatua pia. 

Tunahofu kwakuwa roho inaonekana kama inawepesi usiofaa kututambulisha kama washindi au wamiliki wa kitu, hayo ni mambo ya akili kujitafutia usalama kwa kujihisi ushindi kwenye mfumo inayo uishi. 

Wewe si mawazo, hisia wala nyama tu zinazo endeshwa na mazingira bali ni mwangaza kamili wa uzima na akili kuu iliyojisahau gizani na kujihisi kupoteza maana. Ukiweza kuona hilo ndani yako hutojihisi upo mbali na Mungu bali utamuona muda wote bila upungufu wowote kujihisi nae. 

Nb : Maisha ya kiroho ni kuishi wewe kama roho iliyo huru ndani yako isiyo endeshwa na mawazo wala hisia kwa mifumo yake na wala isiyo pingana na hivyo kwa jinsi ilivyo ni kuwa mwangaza ndani yako unao angaza kila kona ya maisha yako. Lengo kubwa ni kufanya uishi kamili kama roho na si vinginevyo. 






Comments